Msanii wa muziki wa Bongo
Fleva, Godzilla amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumatano majira ya saa 10
alfajiri nyumbani kwao salasala jijini Dar Es Salaam.
Dada wa marehemu, Joyce
Mbunda amethibitisha taarifa hizo ambapo amesema Godzilla alikuwa
anasumbuliwa na tumbo.
Mwili wa Godzilla kwa
sasa umehifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, Dar Es Salaam.


No comments:
Post a Comment