Davido awachana mashabiki wanaomtaka aachane na siasa
Msanii wa muziki nchini
Nigeria, Davido amewachana mashabiki wake wanaomtaka aachane na siasa kwa
kuwambia kuwa yeye kama msanii ana nguvu ya kuzungumzia mambo yote
yanayoonekana hayapo sawa kwenye jamii.
Davido kupitia ukurasa
wake wa Twitter, amesema kuna watu wanamshauri asijihusishe na siasa lakini
yeye amekataa kufanya akiamini kuwa ana sauti kubwa kutetea maovu kwenye jamii.
Davido ni moja ya wasanii
wakubwa nchini Nigeria wanaojihusisha na siasanchinihumo, ambapo mwaka huu
amejitokeza wazi wazi kumpigia upatu Mgombea Urais kwa tiketi ya PDP, Atiku
Abubakar .
Sababu za kifamilia zinamfanya
Davido akipigie upatu chama cha PDP, kwa sababu wazazi wake, mjomba na ndugu
zake wanaunga mkono chama cha PDP na wengine wanagombea ugavana kupitia chama
hicho cha Demokrasia.
Davido amekuwa mstari wa mbele
kusisitiza Wanaigeria kupiga kura na kuzilinda kwenye uchaguzi mkuu Februari
16, mwaka huu.


